1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Kesi ya Saddam yaendelea leo

11 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3w

Kiongozi wa zamani wa Irak, Saddam Hussein, pamoja na washukiwa wenzake saba wamerejea mahakamani leo baada ya kutolewa nje ya mahakama hapo jana.

Saddam amerudia mzozo wa jana na kumuuliza hakimu kwa nini alifukuzwa mahakamani.

Wakati huo huo watu watano wameuwawa leo nchini Irak. Bomu lililokuwa limetegwa ndani ya motokaa limeripuka karibu na kituo cha polisi kusini mashariki mwa Baghdad na kuwaua wapita njia wawili.

Duru za polisi zinasema maofisa wanne wa polisi wamejeruhiwa katika shambulio hilo lililofanywa katika kitongoji cha Ghadeer.

Shambulio lengine la bomu limefanywa mashariki mwa Baghdad katika uwanja wa Mustansiriyah. Wapita njia wawili wameuwawa na watu wengine 16 wamejeruhiwa katika shambulio hilo.

Kaskazini mwa Irak, afisa mmoja wa polisi ameuwawa kwa kupigwa risasi mjini Kirkuk na watu waliokuwa wamejihami na bunduki alipokuwa njiani akielekea kazini.