BAGHDAD: Hali ya kefyu yawekwa mjini Baghdad kufuatia mauaji makubwa | Habari za Ulimwengu | DW | 24.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD: Hali ya kefyu yawekwa mjini Baghdad kufuatia mauaji makubwa

Serikali ya Irak imetangaza hali ya kefyu katika mji mkuu, Baghdad kufuatia mlolongo wa miripuko ya mabomu na makombora ambayo imesababisha vifo vya watu kwa uchache 150 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa. Polisi na maafisa wa wizara ya mambo ya ndani, wamesema miripuko hiyo ilikuwa imepangwa na imetokea moja baada ya mwingine kila dakika 15 katika kitongoji cha Sadr City. Huo ndio mtaa katika mji mkuu Baghdad unaodhibitiwa na wanamgambo wa kiongozi wa kishiha mwenye msimamo mkali, Moqtada al-Sadr.

Katika sehemu nyingine mjini Baghdad, kwa uchache watu watano wameripotiwa kujeruhiwa baada ya watu waliokuwa wamejihami kwa bunduki kulishambulia jengo la wizara ya afya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com