Baada ya Serikali kuregeza baadhi ya sheria, Wacuba sasa kumiliki vifaa vya Elekroniki. | Masuala ya Jamii | DW | 04.04.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Baada ya Serikali kuregeza baadhi ya sheria, Wacuba sasa kumiliki vifaa vya Elekroniki.

Baada ya Serikali kuregeza Sheria nchini Cuba, maduka yameanza kuuza vyombo vya Electroniki vinavyowavutia wananchi wengi.

Rais wa Cuba Raul Castro,kushoto akisalimiana na Katibu Mkuu wa Vatican Mwadhama Tarcisio Kardinali Bertone.

Rais wa Cuba Raul Castro,kushoto akisalimiana na Katibu Mkuu wa Vatican Mwadhama Tarcisio Kardinali Bertone.

Lakini pamoja na kuuzwa kwa wingi kwa vifaa hivyo watu wanashindwa kuvinunua kutokana na uwezo mdogo wa kifedha.

Kundi la Wacuba, kwa mshangao wamekuwa wakitazama katika vioo vya maduka, vyombo vya electroniki kama vile, DVD, Sufuria za kupikia wali kwa umeme, Computa na Maikrowevu.

Vifaa hivyo vimeanza kuruhusiwa kuuzwa kufuatia uamzi wa Serikali wa kuregeza sheria ambapo awali ilikuwa imewabana watu wenye maduka kuviuza kwa wingi.

Ernesto mwenye umri wa miaka 45, anasema yeye binafsi hana Komputa na wala simu ya mkononi, hana uwezo wa kuvinunua kutokana na kiwango kidogo cha mshahara anaopokea na endapo atataka kununua vitu hivyo itambidi kuuza nyumba yake.

Kimsingi Ernesto pamoja na mke wake, endapo wangekuwa na uwezo wa kifedha, katika kipindi cha siku chache tu, wangeweza kununua bidhaa mbalimbali ambavyo Wacuba wengi wamekuwa wakivitamani kwa miaka mingi, kama Komputa na simu za mkononi ambazo zinapendwa na wengi.

Ernesto anasema kufuatia kuregezwa kwa sheria hizo kumefanya maisha yao kuwa huru zaidi lakini yote hayo yanategemea na kiwango cha mshahara wa mtu, Anasema yeye binafsi angeweza kwenda kutembelea hata katika hoteli ya mapumziko nchini humo ambayo kwa miaka kumi sasa imekuwepo kwa ajili ya watalii pekee.

Kwa kutegemea mshahara wake wa mwezi ambao ni Pesos 273 ambazo ni sawa na dola kumi na mbili wakati mshahara wa wastani wa kati wa nchi hiyo ni kati ya dola kumi na saba na ishirini, Ernesto akitaka kwenda kupumzika usiku mmoja tu na mke wake kwenye Hoteli ya kiwanggo cha juu katika nchi hiyo ya Kikomunisti, itambidi AwekE kando mshahara wake wote kwa mwaka mmoja mzima.

Haya ni sehemu ya wimbi la mageuzi yaliyozinduliwa na Raul Castro baada ya kaka yake kuamua kuachia madaraka mwezi Februari mwaka huu.

Wacuba wanaoletewa fedha na jamaa zao wanaoishi nchi za ng’ambo huenda wakawa na uwezo bora zaidi wa kununua vifaa hivyo.

Kwa mujibu wa Mwanauchumi anayeipinga Serikali ya Cuba, Oscar Espinosa Chepe, shida iliyopo kwa hivi sasa ni kwamba Wacuba wengi hawamudu vitu hivyo kwa sababu ya kutegemea mishahara yao tu kitu ambacho kinaungwa mkono pia na Mpinzani mwenzake Manuel Cuesta Morua.

Kwa mtazamo wake, Cuesta Morua, hatua za mageuzi zilizochukuliwa zitaongeza mwanya uliopo kati ya wenye nacho na wasiokuwa na kitu.

Waangalizi wa mambo wanasema kwamba ingawa ni Wacuba wachache wenye uwezo, lakini linabaki kuwa ni suaala la Kisaikolojia kuwa kila mtu ana uhuru wa kununua kile anachokihitaji.

Watu wengine wamekuwa wakidai mabadiliko pia katika sheria za Uhamiaji kwani raia wengi wa Cuba wamekuwa wakipata shida na wanatumia fedha nyingi wanapoomba vibali vya kwenda nje ya nchi yao.

Ofisa wa ngazi ya juu wa nchi hiyo amethibitisha kwamba masuala kama hayo na mengine bado yanaangaliwa lakini pia akabainisha kuwa wasitegemee mabadiliko ya haraka zaidi katika masuala ya Kiuchumi.

Wakati huohuo, tayari Rais Raul Castro wa nchi hiyo ameshaonya kuwa mabadiliko kama hayo yatachukua muda mrefu.

 • Tarehe 04.04.2008
 • Mwandishi Scholastica Mazula
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DcAy
 • Tarehe 04.04.2008
 • Mwandishi Scholastica Mazula
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/DcAy
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com