1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Alonso asema muda wa Bayer Leverkusen kufurahia ushindi bado

5 Aprili 2024

Kocha wa timu ya Bayer Leverkusen, Xabi Alonso, amesema ni mapema mno kuanza kusherehekea ushindi wa Ligi Kuu ya Ujerumani licha ya timu yake kubakisha pointi 13 tu kufika kileleni mwa jedwali.

https://p.dw.com/p/4eTXE
 Xabi Alonso | Bayer Leverkusen
Kocha ya Bayer Leverkusen, Xabi Alonso.Picha: Frank Hoermann/SVEN SIMON/IMAGO

Leverkusen wanaweza kushinda taji lao la kwanza kabisa la Bundesliga baada ya kujulikana matokeo ya mabingwa watetezi Bayern Munich dhidi ya Heidenheim siku ya Jumamosi (Aprili 6).

Soma zaidi: Leverkusen yatinga fainali Kombe la Shirikisho - DFB Pokal

Wiki iliyopita, Kocha Alonso alitangaza kuendelea kusalia Leverkusen msimu ujao licha ya kuwindwa na klabu ya Liverpool na Bayern Munich, akitilia mkazo kwamba wachezaji wake wanaangalia mchezo unaofuata dhidi ya Union Berlin.

Mnamo 2002, Leverkusen walikuwa vinara wa ligi na walifuzu kwa fainali za Kombe la Shirikisho (DFB Pokal) na Ligi ya Mabingwa, lakini walipoteza mataji yote matatu.