ADDIS ABABA : Mengistu apatikana na hatia ya mauaji ya kimbari | Habari za Ulimwengu | DW | 12.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ADDIS ABABA : Mengistu apatikana na hatia ya mauaji ya kimbari

Kiongozi wa zamani wa Ethiopia Mengistu Haile Mariam amekutikana na hatia ya mauaji ya kimbari mwenyewe akiwa hayupo nchini leo hii mwishoni mwa kesi yake ya miaka 12 juu ya utawala wake wa mauaji.

Mengistu ambaye hivi sasa anaishi nchini Zimbabwe alikuwa anatuhumiwa pamoja na wanachama wenzake wa serikali wa ngazi juu kwa kuwauwa maelfu ya watu wakati wa utawala wake wa miaka 17 ambao ulianza kwa kumpinduwa Mfalme Haile Selasie hapo mwaka 1974 na kujumuisha vita,kuwasafisha wapinzani na njaa.

Hakimu Medhen Kiros akitowa hukumu hiyo amesema wajumbe wa Deng baraza la kijeshi la Mengistu ambao walikuwako kwenye mahkama hiyo na wale ambao wanashatakiwa wakiwa hawako walishirikiana kuangamiza kundi la kisiasa na kuuwa watu kiholela .

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com