ABIDJAN: Maandamano ya kumshinikiza rais Laurent Gbagbo ajiuzulu | Habari za Ulimwengu | DW | 16.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABIDJAN: Maandamano ya kumshinikiza rais Laurent Gbagbo ajiuzulu

Maelfu ya watu waliandamana jana katika barabara za mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan, wakidai rais Laurent Gbagbo ajiuzulu.

Kulingana na duru za polisi, waandamanaji zaidi ya 10,000 walikusanyika katika uwanja mojawapo wa michezo mjini Abidjan kwa kuitika mwito wa upinzani. Kwa upande wake upinzani unasema ni watu 40,000 walioshiriki katika maandamano hayo.

Maandamano hayo yalifanyika kufuatia tamko la muakilishi wa Umoja wa mataifa nchini Ivory Coast jumamosi kwamba uchaguzi wa urais uliokuwa ukitarajiwa kufanyika tarehe 31 mwezi huu, huenda ukaahirishwa kwa muda unaoweza kutimia mwaka mzima, ikiwa ni mara ya pili uchaguzi kuahirishwa katika nchi hiyo inaokabiliwa na mzozo wa kisiasa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com