1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky: Ukraine itapokea ndege za kivita kutoka Ufaransa

17 Novemba 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametia saini mpango unaoiruhusu Ukraine, kupokea ndege za kivita aina ya Rafale kutoka Ufaransa, ikiwa ni juhudi za kuimarisha uwezo wake wa kijeshi kupambana na Urusi.

https://p.dw.com/p/53m08
Ufaransa Paris 2025 |Rais Macron na Zelensky
Zelensky: Ukraine itapokea ndege 100 za kivita kutoka Ufaransa ili kuimarisha jeshi lake la ulinziPicha: Sarah Meyssonnier/Pool/AFP

Zelensky yuko ziarani nchini Ufaransa ambako alitia saini mpango huo na kuwa na mazungumzo na rais Emmanuel Macron, wakati kukiwa na ongezeko la mashambulizi makali ya droni na makombora dhidi ya taifa lake kutoka kwa jirani yake Urusi.

Rais huyo wa Ukraine amesema tayari ameagiza ndege 100 za kivita. Ufaransa imethibitisha idadi hiyo bila ya kutoa maelezo zaidi.

Ndani ya Ukraine kwenyewe, shambulizi la Urusi Mashariki mwa mji wa Kharkiv limesababisha mauaji ya watu watatu na kuwajeruhi wengine zaidi ya 10.

Idadi ya waliouwawa huenda ikapanda kutokana na utawala nchini humo kuendelea kupokea taarifa za athari za shamnbulizi hilo.