1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky ashangazwa na matamshi ya Trump kuhusu Ukraine

24 Septemba 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema ameshangazwa na matamshi ya Rais wa Marekani Donald Trump, aliposema anaamini Kiev inaweza kuitwaa tena ardhi yake yote iliyonyakuliwa na Urusi.

https://p.dw.com/p/50ym5
New York, Marekani 2025 | Mkutano kati ya Donald Trump and Volodymyr Zelensky kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Trump asema Ukraine iko katika nafasi nzuri ya kupambana na kushindaPicha: POU/ROPI/picture alliance

Akizungumza Jumanne, Trump alisema Ukraine inapaswa kuchukua hatua sasa wakati ambapo Urusi inakabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi.

Kulingana na Trump, kwa msaada wa Umoja wa Ulaya, Ukraine iko katika nafasi nzuri ya kupambana na kushinda.

Akizungumza baada ya kukutana na Trump pembezoni mwa Hadhara Kuu ya Umoja wa Mataifa, Zelensky amesema kuna maelewano kwamba kiongozi huyo wa Marekani yuko tayari kuhakikisha usalama wa Ukraine baada ya vita kumalizika.

Matamshi hayo ya Trump yanaaashiria mabadiliko makubwa ya msimamo wake ikilinganishwa na ule wa awali.

Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, Kaja Kallas amepongeza mabadiliko ya mtazamo wa Trump katika mzozo wa Urusi na Ukraine.