1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky asaini mkataba wa usalama na Ujerumani

Tatu Karema
16 Februari 2024

Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesaini mkataba wa usalama na Ujerumani ambao Kansela Olaf Scholz ameuita "hatua ya kihistoria", wakati huu mapigano makali yakiendelea kati ya Ukraine na Urusi.

https://p.dw.com/p/4cUPV
Volodymyr Zelensky
Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine.Picha: AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Ujerumani, mkataba huo ni wa thamani ya dola bilioni 1.22 na unalenga kuimarisha ulinzi wa anga na kuongeza silaha za kivita.

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Boris Pistorius, alisema makubaliano hayo ya usalama na Ukraine ni ya kihistoria na kwamba kwa mara ya kwanza "serikali ya Ujerumani inasimama kama nchi mdhamini."

Zelensky pia alitarajiwa kusaini makubaliano kama hayo na Ufaransa jioni ya Jumatano (Februari 16), wakati akisaka msaada wa ziada kwa vikosi vyake vinavyokabiliwa na mashambulizi makali ya Urusi katika uwanja wa mapigano mashariki mwa Ukraine kwa sababu ya uhaba wa silaha.