Wosia wa mwisho wa Maalim Seif Sharif | Matukio ya Afrika | DW | 19.02.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Wosia wa mwisho wa Maalim Seif Sharif

Viongozi wa ACT Wazalendo waelezea kauli na wasia wa marehemu Maalim Seif Sharif kabla ya kifo chake ambaye katika siku za mwisho za uhai wake alitimiza ndoto yake ya kumaliza siasa za chuki na uhasama.

Taarifa za kuumwa Maalim Seif zilitangazwa na Naibu katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zanzibar, Nassor Mazrui wakati akitibiwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja na baadae kusafirishwa jijini Dar es Salaam kupatiwa matibabu zaidi ambapo kuugua kwake kulichukua takriban siku 18 hadi kukatisha uhai wake.

Soma pia: Maalim Seif azikwa Pemba

Wakati Maalim Seif akiwa mgonjwa akipatiwa matibabu alizungumza na viongozi wake akiwemo Nassor Ahmed Mazrui na kuwapa wosia huku akiwasisitizia juu ya kuendeleza umoja ndani ya chama chake pamoja na kufanya kazi kwa ushirikiano chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Maalim Seif alikubali kuungana na serikali na kuwa makamu wa kwanza wa Zrais ZAnzibar, hatua iliyotizamwa kama kuzika tofauti za kisiasa na kuwaunganisha Wazanzibari wote pamoja.

Maalim Seif alikubali kuungana na serikali na kuwa makamu wa kwanza wa Zrais ZAnzibar, hatua iliyotizamwa kama kuzika tofauti za kisiasa na kuwaunganisha Wazanzibari wote pamoja.

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe alizungumza mbele ya Rais wa Zanzibar, Dokta Hussein Ali Mwinyi muda mfupi baada ya kumaliza taratibu zote za mazishi yake na kumueleza namna ambavyo Maalim Seif alimpa kauli yake ya mwisho ambayo kwake ni sawa na kuagana.

Kwa sasa Maalim Seif hayupo tena dunia suala la wananchi ni nani atakayevaa kiatu chake cha kuendeleza yale mazuri aliyopapigania kwa miaka zaidi ya 30, lakini faraja walionayo wananchi wengi ni kuyaelekeza matumaini yao kwa Rais Mwinyi ambaye tayari ameshaahidi mara kadhaa kuyaendeleza Maridhiano ya Kisiasa ya kuwaunganisha Wazanzibari wote.

Sikiliza sauti 39:02

Kipindi cha Maoni: Wasifu na urathi wa marehemu Maalim Seif