1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani ziarani Sweden, Finland

John Juma
13 Februari 2023

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, amekwenda Finland na Sweden kwa ziara ya siku mbili.

https://p.dw.com/p/4NPMr
Belgien | Annalena Baerbock - Rat für Außenbeziehungen in Brüssel
Picha: Kira Hofmann/photothek/IMAGO

Ziara hiyo imetawaliwa na mkwamo wa maombi ya nchi hizo kutaka kujiunga na jumuiya ya kujihami ya NATO na vilevile mjadala kuhusu msaada wa silaha kwa Ukraine. Serikali ya Ujerumani inatafuta kundi la washirika ambao wako tayari kuipa Ukraine vifaru vya kivita.

Katika mji mkuu wa Finland Helsinki, Baerbock atafanya mkutano na waziri wa nje wa nchi hiyo Pekka Haavisto, na pia atazuru kituo cha kiraia cha ulinzi kilichoko chini ya ardhi.

Kesho Jumanne, Baerbock ataendelea na ziara yake hadi Stockholm, mji mkuu wa Sweden.

Sweden na Finland  ziliwasilisha maombi ya kujiunga na NATO karibu mwaka mmoja uliopita.

Lakini ni shuruti nchi zote 30 ambazo ni wanachama wa jumuiya hiyo ziridhie maombi hayo. Kwa sasa Uturuki na Hungary hazijaidhinisha maombi hayo.