1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Watu watatu wauawa kwenye shambulizi la Wahouthi Yemen

Sylvia Mwehozi
7 Machi 2024

Kamandi kuu ya Marekani CENTCOM kwenye kanda ya mashariki ya kati, imesema kuwa watu watatu wameuawa kwenye shambulizi la kombora lililofanywa na waasi wa Kihouthi.

https://p.dw.com/p/4dFJ2
Meli ya True Confidence
Meli ya Ugiriki ya True Confidence iliyoshambuliwaPicha: Dario Bonazza/REUTERS

Kamandi kuu ya Marekani CENTCOM kwenye kanda ya mashariki ya kati, imesema kuwa watu watatu wameuawa kwenye shambulizi la kombora lililofanywa na waasi wa Kihouthi walioilenga meli ya mizigo ya Ugiriki karibu na pwani ya Yemen.

Meli hiyo ya Ugiriki ya True Confidence iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Barbados, ilishambuliwa karibu maili 50 kusini magharibi mwa mji wa bandari wa Aden na kuwaka moto.

Katika taarifa yake kamandi kuu ya Marekani CENTCOM, ilisema kuwa Wahouthi waliishambulia meli ya True Confidence kwa kutumia kombora la masafa jana Jumatano.

Hii ni mara ya kwanza vifo kuripotiwa tangu kulipoanza mashambulizi. Marekani imeapa kuwawajibisha waasi na kuzitaka serikali nyingine kufanya hivyo. Waasi wa Kihouthi wamedai kuhusika na shambulizi hilo katika Ghuba ya Aden.