Migogoro
Wasuluhishi wa Iran kujadiliana na Marekani mjini Geneva
25 Februari 2026
Matangazo
Rais Donald Trump anayeiongezea shinikizo Iran la kufikia makubaliano, mapema Jumanne alisema kwa mara nyingine kwamba kamwe hataruhusu Iran kuwa na silaha ya nyuklia.
Washington na Tehran tayari wamefanya duru mbili za mazungumzo yanayosimamiwa na Oman na yanayolenga kupata makubaliano kuhusu mipango ya nyuklia ya Iran.
Ujerumani yaisihi Iran kuachana na mpango wa silaha za nyuklia
Katika hatua nyingine, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani ameiomba Iran kuachana na mipango hiyo ya nyuklia na makombora ya masafa marefu pamoja na kuacha kuvuruga utulivu wa Mashariki ya Kati.