1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washukiwa wa kundi la RAF wakamatwa Ujerumani

3 Machi 2024

Polisi wamewakamata watu wawili huko Berlin wakati wa msako dhidi ya watu wanaoshukiwa kuhusika katika kundi la zamani la wanamgambo la Red Army Faction (RAF).

https://p.dw.com/p/4d73G
Polisi wakifanya msako dhidi ya washukiwa wawili wa kundi la RAF Ernst-Volker Staub na Burkhard Garweg.Picha: picture alliance/dpa

Msemaji wa polisi kutoka jimbo la Lower Saxony nchini Ujerumani, ambayo ilikuwa ikishiriki katika juhudi hizo, alithibitisha kwamba watu wawili wamekamatwa leo Jumapili lakini bila kutoa majina yao.

Aidha, kitengo cha polisi cha mji wa Berlin kilisema takriban maafisa 130 walishiriki katika msako dhidi ya washukiwa Ernst-Volker Staub na Burkhard Garweg wa kundi la wanamgambo hao.

Msako huo unajiri baada ya kukamatwa kwa mshukiwa mwengine wa kundi la wanamgambo la RAF wiki iliyopita ambaye amekuwa uhamishoni kwa miongo mitatu. Hata hiyvo kundi la RAF lilisambaratika mwaka 1998.

 

RAF