1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakulima wa Ujerumani waandamana nje ya maonyesho ya kilimo

20 Januari 2024

Wakulima wa Ujerumani wamefanya tena maandamano nje ya ukumbi kunakofanyika maonyesho ya Wiki ya Kimataifa ya Kijani ya Berlin yanayowaleta pamoja wadau mbalimbali katika sekta ya kilimo.

https://p.dw.com/p/4bV6k
Matrekta ya wakulima wa Ujerumani wanaondamana mbele ya lango la Brandenburg
Matrekta ya wakulima wa Ujerumani wanaondamana mbele ya lango la BrandenburgPicha: Sean Gallup/Getty Images

Wawakilishi wa muungano unaojiita "Tumechoshwa" waliwasilisha barua ya malalamiko yao kwa waziri wa kilimo Cem Özdemir.

Wakulima hao wanapinga kuondolewa kwa ruzuku ya mafuta kwenye vyombo vya moto vinavyotumika katika kilimo.

Maandamano hayo yalijumuisha wakulima wazee na vijana pamoja na makundi mengine kama vile wafugaji nyuki. Wamehimiza kuwepo kwa sekta ya kilimo iliyoboreshwa, urasimu mdogo na kuimarishwa kwa demokrasia.

Maandamano hayo yalitarajiwa kupita katikati ya mji mkuu Berlin na kukamilika mbele ya ofisi ya Kansela Olaf Scholz.