Wakristo waadhimisha Ijumaa kuu
21 Machi 2008Matangazo
JERUSALEM:
Mahujaji kadhaa wa dini ya kikristo wameshiriki katika maandamano ya njia ya msalaba katika mji mtakatifu wa Jerusalem,huku wenzao maelfu kadhaa duniani wakiadhimisha siku ya leo Ijumaa ya Ijumaa kuu.
Waumini,wengi wao wakiwa wamebeba misalaba mikubwa ya mbao, walitembea katika barabara za mji mkongwe wa Jerusalem,kufuata njia inayofikiriwa kutumiwa na Yesu Kristo akiwa amebeba msalaba na hatimae kusulubiwa na Waroma.
Maandamano hayo yalianzia mahali ambapo inasemekana ndiko aliteswa kwa kupigwa na kuzomewa na kumalizikia katika sehemu za kanisa takatifu iliojengwa mahali wakristo wengi wanakoamini kuwa ndipo yesu Kristo aliposulubiwa na baadae kuzikwa.