1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Wakfu 'tata' wa misaada Gaza watangaza kufunga shughuli zake

25 Novemba 2025

Wakfu wa Misaada ya Kiutu kwenye Ukanda wa Gaza uliokuwa ukiratibiwa na Marekani kwa kushirikiana na Israel unafunga shughuli zake wiki sita baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano kuanza kutekelezwa.

https://p.dw.com/p/54AFF
Gaza 2025 | Wapalestina wakiondoka katika eneo la kugawa chakula linaloratibiwa na Wakfu wa Kibinadamu wa Gaza (GHF) unaoungwa mkono na Marekani na Israel
Wapalestina wakiondoka katika eneo la kugawa chakula linaloratibiwa na Wakfu wa Kibinadamu wa Gaza (GHF) unaoungwa mkono na Marekani na Israel wakiwa na mifuko na magodoro za mbao, karibu na ukanda wa Netsarim katikati mwa Ukanda wa Gaza Agosti 3, 2025.Picha: Eyad Baba/AFP/Getty Images

Wakfu huo uliokuwa na utata, unahitimisha shughuli zake baada ya kusambaza karibu milo milioni 187 kwa wakazi wa ukanda huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakfu huo wa GHF John Acree amesifu mafanikio katika dhamira yao ya kuonyesha kuna namna bora ya kufikisha misaada kwa watu wa Gaza.

GHF ilianza shughuli zake Gaza mwezi Mei baada ya kuzingirwa kwa karibu miezi mitatu na Israel, iliyoishutumu Hamas kwa kuiba misaada ya kibinadamu.

Hata hivyo, kuliripotiwa mara kadhaa mashambulizi dhidi ya raia wa Gaza yaliyosababisha vifo karibu na vituo vya misaada vinavyoratibiwa na wakfu huo.