1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Iran yasema meli 35 zimepita katika Mlango wa Hormuz

22 Mei 2026

Iran imesema leo kuwa, jumla ya meli 35 zimepita katika Mlango Bahari wa Hormuz, ambao ni njia muhimu ya kimkakati kwa biashara ya nishati, ndani ya saa 24 zilizopita.

https://p.dw.com/p/5ECgr
Iran Bandar Abbas 2026 | Meli za makontena zatia nanga katika Mlango-Bahari wa Hormuz
Meli za makontena zatia nanga katika Mlango-Bahari wa HormuzPicha: Amirhosein Khorgooi/ISNA/AP Photo/picture alliance

Iran imesema leo kuwa, jumla ya meli 35 zimepita katika Mlango Bahari wa Hormuz, ambao ni njia muhimu ya kimkakati kwa biashara ya nishati, ndani ya saa 24 zilizopita. Taarifa hiyo imeripotiwa Ijumaa na shirika la utangazaji la serikali ya Iran.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, zoezi hilo limefanyika kwa uratibu na Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC). Awali, jeshi la wanamaji lilikuwa limeripoti siku ya Jumatano kuwa meli 26 zilipita katika mlango huo ndani ya saa 24.

Hata hivyo, kampuni ya takwimu ya kimataifa ya Kpler, ilisema siku ya Ijumaa kuwa ni meli 10 tu zilizopita siku hiyo ya Jumatano.

Kwa mujibu wa jeshi la Iran, miongoni mwa meli zilizopita ni pamoja na meli za mafuta, meli za mizigo pamoja na nyingine za kibiashara.