1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge, Tanzania waipa serikali madaraka makubwa

Sekione Kitojo
30 Januari 2019

Wabunge wa Tanzania wamepitisha mswada wa mabadiliko ambao unatoa madaraka makubwa kwa msajili wa vyama vya siasa ambaye anateuliwa na serikali.

https://p.dw.com/p/3CR13
Tansania Parlament Dodoma - Parlamentsvorsitzende mit Philip Mpango und Premierminister Kassim Majaliwa
Picha: DW/S. Khamis

Bunge  la  Tanzania  limepitisha  mswada  wa  mabadiliko jana  jioni  ambao  unatoa  madaraka  makubwa  kwa msajili  wa  vyama  vya  siasa  ambaye  anateuliwa  na serikali, hatua  ambayo  wabunge  wa  upinzani  wanasema itaimarisha  utawala  wa  chama  kimoja.

Serikali  ya  Rais John Pombe  Magufuli tayari  imekwisha piga  marufuku baadhi  ya  magazeti, kuzuwia  mikutano ya  vyama  vya  upinzani  na  kuwakamata  wanachama kadhaa  wa  vyama  hivyo, pamoja  na  kuingilia  kati  mara kwa  mara  kwa  serikali  katika  sekta  muhimu  kama madini  na  kilimo, na  kudhoofisha  uwekezaji  katika  nchi hiyo  yenye  uchumi  mkubwa  wa  tatu  katika  eneo  hilo.

Mabadiliko  hayo yanampa msajili  anayeongozwa  na serikali  madaraka  makubwa  kuweza  kukifuta chama  na kutoa  hukumu  ya  hadi  mwaka  mmoja  jela  kwa  mtu yeyote anayefanya harakati za  elimu  ya  raia  ambayo haikuidhinishwa, kwa  mfano utaratibu  wa  kujiandikisha kupiga  kura.

Viongozi  wa  upinzani wanasema mabadiliko  hayo  ya sheria yatanya shughuli  za  kisiasa  kuwa  uhalifu na kuigeuza Tanzania  kuwa  ya  chama  kimoja.