1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tanzania: Vyombo vya habari vya kimataifa vizingatie maadili

23 Novemba 2025

Msemaji Mkuu wa serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa amevituhumu vyombo vya habari vya kimataifa kuchapisha habari zinazoegemea upande mmoja.

https://p.dw.com/p/544kJ
Tansania | Gerson Msigwa msemaji wa serikali Tanzania
Msemaji wa serikali ya Tanzania Gerson Msigwa amevitaka vyombo vya habari vya Kimataifa vizingatie maadili vinaporipoti matukio ya Tanzania Picha: Privat

Akizungumza na vyombo vya habari katika kituo cha mkutano cha Kimataifa mjini Dar es Salaam,  Msigwa amedai kuwa vyombo hivyo vya habari kama CNN, DW, Al Jazeera na BBC vinachapisha taarifa za upande mmoja na baadae kudai kuwa juhudi za kuwatafuta maafisa wa serikali zimefeli.

DW mara zote hufanya kila juhudi kupata maoni ya kila upande.

Madai ya msigwa yamejiri siku chache baada ya chombo cha habari cha Kimataifa CNN kuchapisha makala fupi iliyoonyesha mauaji yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, uliompa ushindi Rais Samia Suluhu Hassan.

Hata hivyo serikali hiyo imesema bado inachambua na kuhakiki maudhui yaliyomo katika makala hiyo.