1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Vurugu za magenge zaendelea katika mji mkuu Port-au-Prince

21 Machi 2024

Magenge yenye silaha yamefanya mashambulizi mapya katika viunga vya mji mkuu Port-au-Prince huku milio ya risasi ikisika usiku kucha karibu na mji mkuu huo.

https://p.dw.com/p/4dxO6
Watu wakichoma takataka karibu na miili 10 ya watu waliofariki viungani mwa mji mkuu Port-au-Prince
Watu wakichoma takataka karibu na miili 10 ya watu waliofariki viungani mwa mji mkuu Port-au-PrincePicha: Guerinault Louis/Anadolu/picture alliance

Waandishi wa habari wa shirika la Associated Press wameripoti kuona miili ya watu watano barabarani.

Mashambulizi hayo yanatokea huku wizara ya mambo ya nje ya Marekani ikitangaza kuwa imekamilisha uhamisho wake wa kwanza wa raia wa Marekani kutoka Port-au-Prince.

Zaidi ya Wamarekani 15 wamesafirishwa kwa ndege hadi Santo Domingo, mji mkuu wa Jamhuri ya Dominica.

Soma pia: Watu 10 wauawa katika kiunga cha Port-au-Prince 

Wizara hiyo ya mambo ya nje ya Marekani imeendelea kueleza kuwa zaidi ya raia 30 wa Marekani watahamishwa kutoka Port-au-Prince kila siku kwa kutumia helikopta.

Vurugu za magenge nchini Haiti zimelazimisha kufungwa kwa benki, shule na kuathiri shughuli nyengine za kawaida.