Antonio Costa, Ursula Von der Leyen wawasili India
25 Januari 2026
Matangazo
Costa na rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen ni wageni wakuu wa maadhimisho ya mwaka huu ya Jamhuri ya India katika jiji la New Delhi yatakayofanyika Jumatatu kabla ya mkutano wa kilele wa 16 wa Umoja wa Ulaya na India.
Mkataba mkubwa wa biashara huria kusainiwa Jumanne
Mkutano wenyewe utafanyika Jumanne wiki ijayo ambapo pande hizo mbili zinatarajiwa kusaini mkataba huo, unaoelezewa kuwa mkubwa kuliko mikataba mingine yote.
Mkutano huo utakuwa fursa ya kujenga ushirikiano wa kimkakati kati ya Umoja wa Ulaya na India na unalenga kuimarisha zaidi ushirikiano kwenye sera muhimu.