1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viogozi wa dunia waomboleza kifo cha Rais wa Iran

20 Mei 2024

Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel ametoa salamu zake za rambirambi kwa Iran, baada ya tangazo la kifo cha rais wa taifa hilo Ebrahim Raisi katika ajali ya helikopta.

https://p.dw.com/p/4g4B6
Tehran, Iran | Mwanamke akilia baada ya taarifa za kifo cha Ebrahim Raisi.
Mwanamke wa raia wa Iran, akilia kwa uchungu baada ya taarifa za kurhibitishwa kwa kifo cha Rais wa Iran Ebrahim Raisi.Picha: Majid Asgaripour/Wana News Agency via REUTERS

Michel amesema anatoa pole kwa familia ya raisi na maafisa wengine 9 wa serikali walioangamia katika ajali hiyo.

Viongozi wengine wa dunia pia wameungana na Michel kutoa pole zao kwa Iran baada ya rais wake pamoja na waziri wa mambo ya nje kufa katika ajali hiyo

Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim amesema amesikitishwa na vifo vya viongozi hao, akisema bado Malaysia itaendelea kuimarisha mahusiano yake na Iran, kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya watu wao na dunia ya kiislamu.

Soma pia:Helikopta iliyombeba rais wa Iran yapata ajali, haijulikani ilipo

Rais Vladimir Puin wa Urusi,  amesema Raisi alikuwa  kiongozi mahiri aliyejitolea kuitumikia nchi yake na amechangia pia kuimarisha mahusiano ya mataifa hayo mawili. 

Naye rais wa Uturuki Tayyip Erdogan, amesema anamkumbuka rais Ebrahim Raisi kwa heshima kubwa kutokana na juhudi zake za kuleta amani kwa watu wa Iran na kanda nzima. 

Wengine waliotuma salamau zao za pole ni pamoja na Jumuiya ya nchi za kiarabu, Japan, Italia, Pakistan, Srilanka, Jordan Qatar na India.