Vienna. Iran na IAEA zafikia makubaliano. | Habari za Ulimwengu | DW | 14.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Vienna. Iran na IAEA zafikia makubaliano.

Shirika la umoja wa mataifa la nishati ya atomic limesema kuwa limefikia makubaliano na Iran ambayo yanatatua masuala yaliyobaki juu ya majaribio ya hapo kabla ya Plutonium ya nchi hiyo.

Kufuatia mazungumzo ya siku mbili mjini Tehran , shirika hilo la kimataifa la nishati ya Atomic limesema kuwa limepanga wachunguzi wa IAEA kutembelea kinu cha kinuklia cha utafiti wa maji maji mazito katika eneo la Arak ifikapo mwishoni mwa mwezi Julai.

Uamuzi juu ya kushughulikia usalama katika kinu cha urutubishaji wa madini ya Uranium katika kituo cha Natanz unatarajiwa kufikiwa mapema mwezi wa August.

Mataifa ya magharibi yanashaka kuwa mpango wa kinuklia wa Iran ni wa kuunda silaha za kinuklia. Iran inasema kuwa inataka teknolojia hiyo ya kinuklia kwa ajili ya kuzalisha umeme.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com