VATICAN CITY : Papa anasema dunia inapuuza wenye dhiki | Habari za Ulimwengu | DW | 26.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

VATICAN CITY : Papa anasema dunia inapuuza wenye dhiki

Katika sala ya desturi ijulikanayo kama Urbi et Orbi ya kuibariki dunia Papa Benedikt 16 ametuma ujumbe akiwaeleza binaadamu wasifikirie kama wanaweza kuishi bila ya Mungu.

Papa amewaambia maelfu ya waumini katika Uwanja wa Kanisa la St.Peter hapo jana kwamba dunia ikiwa chini ya msingi wa kujali matumizi imeendelea kupuuza kilio cha moyoni cha watu wanaokufa kutokana na njaa,kiu,magonjwa,umaskini na vita.

Amesema licha ya kuwepo kwa mafanikio katika dunia ya kisasa ulimwengu bado unaedelea kuhitaji mno Muokozi.Benedict pia ametowa wito wa kufikiwa kwa ufumbuzi kwa mizozo duniani kote hususan Mashariki ya Kati na Afrika.

Na katika ujumbe tafauti kwa jamii ndogo ya Wakristo wanaoishi Mashariki ya Kati Papa amesema anatumai kutembelea Ardhi hiyo Takatifu wakati hali itakaporuhusu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com