1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uwanja wa ndege mjini Port-au-Prince wafunguliwa tena

Sylvia Mwehozi
21 Mei 2024

Uwanja wa ndege wa kimataifa katika mji mkuu wa Haiti wa Port-au-Prince umefunguliwa tena jana kwa safari za kawaida, takribani miezi miwili na nusu baada ya kufungwa kufuatia ghasia za magenge ya kihalifu.

https://p.dw.com/p/4g5A6
Haiti | Port-au-Prince
Wanajeshi wakishika doria mjini Port-au-PrincePicha: Odelyn Joseph/AP/picture alliance

Uwanja wa ndege wa kimataifa katika mji mkuu wa Haiti wa Port-au-Prince umefunguliwa tena jana kwa safari za kawaida, takribani miezi miwili na nusu baada ya kufungwa kufuatia ghasia za magenge ya kihalifu.

Hadi sasa ni shirika la ndege la Haiti ambalo limetangaza kuanza tena safari zake kati ya Port-au-Prince na Miami na Florida. Uwanja huo wa ndege wa kimataifa ulifungwa kwa safari za abiria mapema mwezi Machi, kufuatia mashambulizi yaliyoratibiwa na magenge ya kihalifu yaliyokuwa na dhamira ya kumwondoa madarakani waziri mkuu Ariel Henry.

Bandari kuu nchini humo bado imefungwa. Magenge ya kihalifu yanadhibiti karibu asilimia 80 ya mji mkuu. Mashirika ya ndege ya Marekani yanatarajiwa kuanza tena safari katika uwanja huo mwishoni mwa mwezi huu.