Uturuki na Croatia | Michezo | DW | 20.06.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Uturuki na Croatia

Uturuki na Croatia zinaania leo tiketi yao ya nusu-finali ya kombe la Ulaya baada ya jana Ujerumani kuitoa Ureno 3:2.

Baada ya Ujerumani -mabingwa mara tatu wa Ulaya kukata jana tiketi ya kwanza ya nusu-finali ya kombe la Ulaya,leo ni zamu ya waturuki na wacroatia kukata yao:

Polsi ya Austria imesema haitapata usingizi usiku huu kwavile mashabiki 200.000 wa timu hizo 2 watauvamia mji wao wa Vienna kuzishangiria timu zao.Usiku wa jana nchini Ujerumani pia maalfu ya wajerumani wakipepea bendera zao kwenye magari walitamba mitaani wakisherehekea kufufuka kwa timu yao kufuatia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ureno.Ureno ikifuta machozi ya kuaga kombe la Ulaya inatazamia kumtangaza kocha wake mpya atakaejaza pengo la Mbrazil Felipe Scolari mwezi ujao.

►◄

Msemaji wa polisi mjini Vienna, alisema leo timu yoyote kati ya hizi mbili-Croatia au Uturuki ikishinda leo jioni, polisi hawatalala .Kwani, mashabiki wao waliojazana mjini Vienna kwa mechi hiyo watakuwa na party kushangiria.Vienna, una idadi kubwa ya wakaazi wa kituruki lakini pia wacroatia watakaoungana na mashabiki wengine wa kituruki na ki-croatia watakaowasili kutoka nchi jirani-Ujerumani na kutoká Uturuki na croa binafsi.

Kiasi cha polisi 4,600 watashika zamu wakisaidiwa na wachunguzi 15 wa ki-croatia na 4 wa kituruki wa kutambulisha wahuni wazusha fujo.

Wakati Croatia ilizusha msangao ilipoitimua Ujerumani 2:1 katika mpambano wake wa kwanza na mwishoe ikaparamia killeni mwa kundi lake katika duru ya kwanza,Uturuki mara 2 ilitoka nyuma na kuibuka mshindi dakika za mwisho.

Mshindi leo ana miadi na Ujerumani jumatano ijayo kwa nusu-finali ya kwanza.Ikiwa Croatia itaitoa leo Uturuki,Croatia itakumbana tena na Ujerumani,ingawa itakua timu tofauti na ile waliocheza nayo duru ya kwanza.

Changamoto kati ya Ujerumani na Uturuki,itaandamana na jazba kubwa:kwani, kuna kiasi cha waturuki milioni 2.5 Ujerumani na timu yao itakua kana kwamba inacheza nyumbani.

Ikiwa wageni waturuki watatamba na kuwatoa wajerumani,basi sijui hali itakuaje Berlin, wanakoishi waturuki kiasi cha laki moja.

Maalfu ya wajerumani jana walipepea bendera zao kwenye motokaa wakipiga horni kushangiria ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ureno.Ilikua hivyo, Berlin,Hamburg,Munich na hata Cologne-miji mikuu ya Ujerumani.

Hata kanzela Angela Merkel aliangalia changamoto ya jana akikwepa kidogo mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulya huko Brussels.

Polisi ya Ujerumani iliarufu mashabiki 14.000 walijikusanya katika barabara kuu la Berlin-Kurfuerstendamm,wakicheza ngoma na kuzuwia misafara.

Kesho jumamosi ni zamu ya Holland kupambana na Urusi,kuania tiketi nyengine ya nusu-finali huko makocha 2 wadachi wakiongoza timu zao 2-van Basten na Guus Hiddink.Itali inarudi uwanjani jumapili ikicheza na Spian.