1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani wadai kuwepo udanganyifu katika uchaguzi

Tatu Karema
28 Oktoba 2020

Mgombea wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu ametishia maandamano makubwa iwapo kile anachokidai kuwa dosari za uchaguzi kitaendelea

https://p.dw.com/p/3kXsZ
Tansania Singida | Wahlen | Tundu Antiphas Lissu
Picha: Said Khamis/DW

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amelaani kile ambacho amedai ni dosari nyingi katika vituo mbalimbali vya upigaji kura wakati wa uchaguzi mkuu leo. Lissu ameonya kuwa ataitisha maandamano makubwa ikiwa dosari hizo zitaendelea.

Lissu ambaye alinusurika kifo miaka mitatu iliyopita baada ya kupigwa risasi 16 anatoana jasho na Rais Magufuli kwenye kinyang'anyiro hicho.

Lissu ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwaripoti zaonyesha dosari nyingi kwa njia ya kuwazuia mawakala wao kuingia katika vituo vya upigaji kura. Amedai pia kulikuwa na vijisanduku vya kura ambavyo tayari vilishajazwa kura ndani.

Rais Magufuli ambaye amekuwa madarakani tangu 2015 anatarajiwa kuibuka mshindi, licha ya kurudi kwa Lissu aliyekuwa nje ya nchi kwa muda mrefu akitibiwa.