1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Wanawake, watoto wako hatarini katika vizuizi vya Libya

Iddi Ssessanga
13 Oktoba 2021

Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, limeonya kuwa wanawake na watoto wasiopungua 1,000 walioko vizuizini katika mji mkuu wa Libya wako katika hatari ya papo hapo.

https://p.dw.com/p/41cUI
Libyen Auffanglager für Flüchtlinge | Ganzour bei Tripolis
Picha: Getty Images/AFP/M. Turkia

UNICEF imesema katika taarifa yake hapo jana, kwamba karibu wanawake 751 na watoto 255 walikuwa miongoni mwa maelfu ya wahamiaji na watafuta hifadhi waliokamatwa katika misako ya mjini Tripoli mwezi huu, na kuongeza kuwa watoto watoto wasioambatana na watu wazima na vichaga visivyopungua 30 ni miongoni mwa wanaoshikiliwa.

Taarifa ya shirika hilo imesema usalama na ustawi wa wanawake na watoto hao viko hatarini.

Mamlaka nchini Libya ziliendesha msako mkubwa mjini Tripoli, ukiwalenga hasa wahamiaji haramu mapema mwezi huu.

Shirika la hisani la Madaktari wasio na Mipaka, lilisema wahamiaji wasiopungua 5,000 na wakimbizi walikamatwa kupitia misako hiyo ya vurugu na kuzuwiwa katika mazingira duni.

Mtu mmoja aliripotiwa kuuawa na wengine 15 kujeruhiwa, kwa mujibu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya.