Tunatumia 'cookies' ili kuboresha huduma zetu kwako. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana katika sera yetu ya faragha.
UNICEF ni shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto na wanawake katika mataifa yanayoendelea.
Kazi kubwa zaidi za UNICEF zinakuwa mashinani, na ina wafanyakazi katika mataifa na maeneo zaidi ya 190 duniani kote.
Shirika la Kuwahudumia Watoto la Umoja wa Mataifa limeyashutumu vikali mataifa tajiri ulimwenguni kwa kuhatarisha maisha ya watoto kote duniani kutokana na uzalishaji mkubwa wa gesi za sumu zinazoathiri afya zao.
Shirika la afya ulimwenguni, WHO limearifu kuhusu visa 228 vinavyohisiwa kuwa ni maambukizi ya homa ya ini kwa watoto ambayo hata hivyo bado hayajajulikana chanzo chake.
Siku 47 tangu Urusi ilipoivamia Ukraine, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky asema maelfu ya watu wameuawa katika mji wa pwani wa Mariupol na kwamba Urusi inapanga kufanya mashambulizi mapya katika mji huo wa bandari.
Takriban watoto 46 waliuwawa au kujeruhiwa kwenye vita nchini Yemen katika kipindi cha miezi miwili ya mwaka wa mwaka 2022 wakati mapigano yakiongezeka
Shirika la afya duniani WHO na lile la kuhudumia watoto UNCEF, yamezituhumu kampuni za maziwa kwa kuwalenga wanawake wajawazito na kina mama wadogo kwa kutumia mbinu za uuzaji zisizo za kimaadili.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amebadili msimamo wake kuhusu kufunguliwa kwa shule nchini humo, akisema shule zitafunguliwa licha ya masharti aliyoyatoa.
Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, limeonya kuwa wanawake na watoto wasiopungua 1,000 walioko vizuizini katika mji mkuu wa Libya wako katika hatari ya papo hapo.
Umoja wa Mataifa umesema ulimwengu kwa mara ya kwanza umeshuhudia ongezeko la idadi ya watoto wanaofanyishwa kazi katika kipindi cha miongo miwili. Idadi ya watoto wanaotumikishwa ilifikia milioni 160 mwanzoni mwa 2020
Athari kubwa za janga la Covid-19 kwa wanawake katika baadhi ya mataifa huenda zikasababisha ndoa milioni 10 zaidi za watoto katika muongo huu, kwa mujibu wa tathmini iliyotolewa na UNICEF Jumatatu.
Serikali ya Tanzania imetoa onyo kali dhidi ya wale wanaotoa na kusambaza taarifa kuhusiana na magonjwa ya mlipuko ikiwamo janga la maambukizi ya virusi vya corona.
Shirika la UNICEF limesema Sudan Kusini inakabiliwa na tatizo la uhaba wa maji safi ya kunywa na pia uhaba wa vyoo jambo ambalo huenda likasababisha mripuko wa maradhi ya hatari mwaka 2021.
Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, limeonya juu ya kile linachosema ni "kizazi kilichopotea", katika wakati ambapo virusi vya corona vikiendelea kuathiri elimu, lishe na afya za watoto ulimwenguni.
Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limezionya nchi za mashariki na kusini mwa Afrika kuwa ziko katika hatari ya kupoteza kizazi ikiwa hazitofunguwa skuli kwa ajili ya masomo kufuatia mripuko wa COVID-19.
Utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Watoto, UNICEF na Shirika la kimataifa la kuwasaidia watoto la Save the children umeonyesha janga la COVID-19 limewatumbukiza watoto milioni 150 kwenye umasikini.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto, Unicef limeonya kwamba mamilioni ya watoto huenda wakatumbukia kwenye janga la njaa,huku mripuko wa virusi vya Corona ukiwa umesambaa nchini humo.
Congo inakabiliwa na ugonjwa mpya wa Ebola huko kaskazini magharibi mwa nchi. Ni kwa mara ya saba sasa tangu mwaka 2007 Congo kukumbwa na ugonjwa wa Ebola, lakini taifa hilo imejiandaa vyema mara hii ili kukabiliana nao.