1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

AU na EU zaahidiana kuendeleza ushirikiano

26 Novemba 2025

Nchi za Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika zimesisitiza umuhimu wa kuwa na ushirikiano wa karibu ili kufungua milango ya fursa zaidi kati yao.

https://p.dw.com/p/54I14
Luanda, Angola
Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika Luanda, AngolaPicha: Eva Krafczyk/dpa/picture alliance

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumanne mwishoni mwa mkutano wa kilele uliofanyika Luanda nchini Angola, nchi hizo zimesisitiza dhamira yao katika kushughulikia athari za mabadiliko ya tabianchi, na kukuza matumizi ya nishati jadidifu barani Afrika.

Amani na utatuzi wa mizozo vyatiliwa mkazo

Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa amesema pande hizo mbili zimetilia pia mkazo umuhimu wa kuitatua mizozo kote duniani amesema, "Tunasisitiza tena msimamo wetu usioyumba katika kupata amani ya kudumu inayozingatia haki Ukraine, katika eneo linalokaliwa kwa mabavu la Palestina, Sudan, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sahel, Somalia na katika maeneo mengine yenye mizozo kote duniani."

Pande zote za mazungumzo hayo zimesisitiza tena pia dhamira yao ya kudumisha demokrasia, utawala bora, utawala wa sheria, haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari.