1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Ukraine yasema ilidungua droni mbili kati ya tatu za Urusi

1 Aprili 2024

Jeshi la Ukraine limesema kikosi chake cha anga kilidungua droni mbili kati ya tatu aina ya Shahed, zilizorushwa na Urusi usiku wa kuamkia leo.

https://p.dw.com/p/4eJM9
Iran Tehran | Droni aina ya Shahed
Droni aina ya ShahedPicha: Sobhan Farajvan/Pacific Press/picture alliance

Jeshi la Ukraine hata hivyo halijatoa taarifa zaidi kuhusu shambulizi hilo katika taarifa yake iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Katika taarifa tofauti, wizara ya nishati ya Ukraine imesema vifaa katika kituo kidogo cha umeme kwenye mkoa wa kusini wa Zaporizhzhia vimeharibiwa kufuatia shambulizi la droni.

Soma pia: Urusi yashambulia maeneo mbalimbali nchini Ukraine 

Hata hivyo haikufafanua aina gani ya droni ilitumika.

Usiku wa Jumatatu ulikuwa tulivu kiasi kwa Ukraine kufuatia mkururo wa mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati ya nchi hiyo, ambayo Urusi ilizidisha zaidi ya wiki moja iliyopita.