1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Urusi yashambulia maeneo mbalimbali nchini Ukraine

29 Machi 2024

Vikosi vya Urusi vimeendeleza mashambulizi katika maeneo mbalimbali nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4eF3J
Dnipro- Vita vya Urusi nchini Ukraine
Miundombinu ya kuzalisha umeme ikishambuliwa huko Dnipro nchini Ukraine mnamo Machi 2024Picha: Denys Shmyha/Telegram/AP/picture alliance

Mapema Ijumaa, Gavana wa mkoa wa Dnipro Serhiy Lysak amesema mtu mmoja amejeruhiwa na miundombinu kadhaa ilishambuliwa katika wilaya ya Kamianske.

Mashambulizi mengine yameripotiwa mashariki mwa Ukraine ambako mapigano makali yameshuhudiwa karibu na miji iliyoharibiwa vibaya na vita ya Avdiivka na Bakhmut. Kamandi kuu ya jeshi la Kiev imesema jumla ya sehemu 48 huko Kharkiv zimeshuhudia mapigano makali.

Soma pia: Ukraine kuimarisha ulinzi kufuatia ongezeko la mashambulizi ya Urusi

Hayo yanajiri wakati Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amezungumza kwa njia ya simu na  Spika wa Bunge la Marekani Mike Johnson na amemueleza umuhimu wa kupokea msaada wa kijeshi uliozuiliwa wa dola bilioni 60 ili kukabiliana na uvamizi wa Urusi.