1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miito yatolewa kumtaka kocha Nagelsmann aachie ngazi

30 Juni 2026

Ujerumani imefungishwa virago kuondoka kwenye Kombe la Dunia 2026 baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 4-3 na Paraguay

https://p.dw.com/p/5GIlD
Mechi kati ya Ujerumani dhidi ya  Paraguay imewavunja moyo mashabiki wa Ujerumani kote duniani
Mechi kati ya Ujerumani dhidi ya Paraguay imewavunja moyo mashabiki wa Ujerumani kote dunianiPicha: Peter Cziborra/REUTERS

Ujerumani imeondolewa kwenye Kombe la Dunia 2026 baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 4-3 na Paraguaykufuatia sare ya bao 1-1 iliyodumu hadi dakika 120 katika hatua ya 32 bora.

Baada ya kipigo hicho, nahodha wa zamani wa Ujerumani, Lothar Matthäus, amesema ni wakati wa kocha, Julian Nagelsmann, kuondoka, akidai timu inahitaji mwanzo mpya baada ya kushindwa kuvuka hatua za awali kwa mara ya tatu mfululizo kwenye Kombe la Dunia. Paraguay ilitangulia kupata bao la Julio Enciso kabla ya Kai Havertz kuisawazishia Ujerumani.Kombe la Dunia 2026: Messi ang'ara, Afrika yaandika historia

Wakati huo huo, timu ya Afrika, Morocco imeandika historia kwa kutinga hatua ya 16 bora baada ya kuiondoa Uholanzi kwa mikwaju ya penalti. Ushindi huo uliibua shamrashamra kubwa katika mji wa The Hague nchini Uholanzi, ambako maelfu ya watu wenye asili ya Morocco walijitokeza kusherehekea mitaani. Hata hivyo, baadaye polisi wa kutuliza ghasia walitumia magari ya maji na virungu kuwatawanya baadhi ya waliokuwa wakisherehekea, huku watu kadhaa wakikamatwa baada ya vurugu kuzuka.