Ubalozi wa Ujerumani mjini Khartoum washambuliwa
14 Septemba 2012Matangazo
Mjini Khartoum wafuasi wasiopungua elfu tano wa itikadi kali ya dini ya kiislamu wamezivamia ofisi za balozi za Uingereza na Ujerumani na kuutia moto ubalozi wa Ujerumani. Kwa mujibu wa mashahidi na maripota wa shirika la habari la Uingereza, Reuters, na lile la Ufaransa, AFP, waandamanaji waliojaa hasira waliparamia jengo la ubalozi wa Ujerumani na kupandisha bendera ya itikadi kali badala ya ile ya Ujerumani.
"Watumishi wa ubalozi wako salama" amesema waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle, aliyewataka maafisa wa serikali ya mjini Khartoum wachukue hatua zinazohitajika kudhamini usalama wa wanadiplomasia.
Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP/Reuters
Mhariri:Josephat Charo