Tume ya muda ya uchaguzi Kenya imejiandaa kwa kura ya maoni Agosti 4
2 Agosti 2010Matangazo
Tume ya uchaguzi nchini Kenya imo katika maandalizi ya mwisho kabla tayari kwa kura ya maoni itakayopigwa Jumatano ijayo, kuhusu katiba mpya ya nchi hiyo. Tume hiyo imesema kwamba kuanzia leo usiku hakutaruhusiwa mipango yoyote ya kampeni hadharani wala faraghani.
Kwa mara ya kwanza katika uchaguzi wa kitaifa, tume hiyo itatumia mbinu ya simu ya mkononi kupokea matokeo kutoka katikavituo vyote vya kupigia kura ili kuharakisha zoezi hilo. Peter Moss alizungumza na kamishna wa tume hiyo ya uchaguzi Winnie Guchu na alianza kwa kueleza mikakati yao ya kujitayarisha.
Mwandishi, Peter Moss
Mhariri, Abdul-Rahman Mohamed