1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump kubatilisha mkataba wa silaha wa Marekani na Urusi

Oumilkheir Hamidou Inlandspresse
22 Oktoba 2018

Kwa mara nyengine tena rais wa Marekani Donald Trump ameushitua ulimwengu alipotangaza azma ya kujitoa katika mkataba unaositisha mashindano ya kujirundukia silaha kati ya madola makuu

https://p.dw.com/p/36w1Y
USA Präsident Donald Trump Wahlkampf | Elko Regional Airport in Elko Nevada
Picha: Reuters/J. Ernst

Azma ya rais wa Marekani Donald Trump ya kubatilisha mkataba uliofikiwa miongo kadhaa iliyopita pamoja na Urusi dhidi ya kutengeneza makombora yenye uwezo wa kushambulia hadi umbali wa kilomita 5500, kisa cha kuuliwa mwandishi habari wa Saudi Arabia Jamal Khashoggi na maandamano ya London dhidi ya mpango wa kujitia Uingereza katika Umoja wa Ulaya-Brexit ni miongoni mwa mada magazetini.

Tunaanzia Washington ambako kwa mara nyengine tena rais wa Marekani Donald Trump ameushitua ulimwengu alipotangaza azma ya kujitoa katika mkataba unaositisha mashindano ya kujirundukia silaha kati ya madola makuu. Gazeti la Mannheimer Morgen linaandika:

"Kama ilivyotokea katika mkataba kuhusu biashara, mabadiliko ya tabianchi na haki za binaadam, Donald Trump anaonyesha amedhamiria kubatilisha makubaliano yaliyoko. Huu si mkakati bali kosa lenye madhara makubwa."

Trump atishia kukabtilisha mkataba wa kupunguza silaha

Gazeti la mjini Freiburg,"Badische Zeitung" linasema "azma ya Trump" si kitu kipya."Gazeti linaendelea kuandika: "Ndio mambo anayoyapenda hayo. Wakati viongozi wengine wanatathmini , wanapima na kuhimiza mazungumzo yafanyike, yeye anajiamulia kufumba na kufumbua. Mkataba wa kupunguza silaha ni mojawapo ya nguzo za usalama barani Ulaya. Mkataba huo uliofikiwa  mwaka 1987 kati ya Ronald Reagan na Michael Gorbatchov unapiga marufuku kumiliki makombora ya nuklea ya masafa mafupi na ya wastani.Trump anahisi Marekani inaweza kufaidika zaidi pindi akiubatilisha."

 Biashara ya silaha na Saudi Arabia istishwe

Sauti zinazidi kupazwa nchini Ujerumani kudai biashara ya silaha pamoja na Saudi Arabia isitishwe hasa baada ya Ryadh kuungama hatimae kwamba Khashoggi ameuliwa katika ubalozi wake mdogo mjini Istanbul, Gazeti la "Rhein Necker-Zeitung linaandika: "Ujerumani inaiuzia silaha Saudi Arabia. Lakini sasa tangu mwandishi habari anaeikosoa nchi hiyo ya kifalme kuuliwa kikatili kabisa, mjadala umezuka kama ni sawa kuendeleza biashara hiyo. Nchini Ujerumani na sio Marekani ambako Donald Trump anatanguliza mbele zaidi vipi ataokoa nafasi zaidi za kazi. Ujerumani haiwezi kuizuwia Marekani isiipatia Saudi Arabia silaha. Lakini inaweza yenyewe kuachilia mbali kuwapatia zana za vita waimla wa nchi hiyo. Na mkuu wa kampuni la Siemens anaweza kukipa kisogo kiti chake mjini Riyadh hata kama nafasi za kazi zitapungua."

 

Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman