Taifa Stars kukipiga na Nigeria mechi ya kwanza AFCON
22 Desemba 2025
Matangazo
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kesho Disemba 23 itatupa karata yake ya kwanza dhidi ya Nigeria katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) inakayofanyika nchini Morocco
Taifa stars imepangwa kundi C lenye timu ya Uganda,Tunisia,na Nigeria
Ikumbukwe kuwa AFCON ya Morocco itakuwa mara ya nne kwa Taifa Stars kushiriki michuano hiyo, baada ya kushiriki awali mwaka 1980, 2019 na 2023. Hivyo, mchezo wa kesho dhidi ya Nigeria sio tu mwanzo wa mashindano, bali ni mwendelezo wa historia ya Tanzania katika jukwaa la soka la Afrika.
Lakini pamoja na kushiriki huko kwa mara tatu mfululizo,Taifa Stars haijawahi kupata ushindi katika mechi yeyote ya michuano hii ingawa pengine mara hii inaweza kupata ushindi huko Morocco.