Algeria yaifunga Uholanzi 1-0, maandalizi ya Kombe la Dunia
4 Juni 2026
Matangazo
Kinyume na matarajio, bao zuri lililofungwa dakika ya 86 na Hadj Moussa kwa shuti la mguu wa kushoto lililopinda na kuingia juu ya kona liliihakikishia Algeria ushindi katika mchezo ambao kwa kiasi kikubwa ulidhibitiwa na Uholanzi. Uholanzi walizuiwa mara kwa mara na kipa wa Algeria, Luca Zidane, mwana wa gwiji wa zamani wa Ufaransa, Zinedine Zidane. Kipa huyo mwenye umri wa miaka 28, anayecheza katika klabu ya Granada ya daraja la pili nchini Hispania, ameongeza nafasi yake ya kujumuishwa katika kikosi cha mwisho baada ya Algeriakutaja makipa wanne katika kikosi cha awali, huku watatu tu wakitarajiwa kwenda Kombe la Dunia litakalofanyika Amerika Kaskazini kuanzia tarehe 11 Juni hadi 19 Julai.