Silaha za Libya zatapakaa Mali, Syria | Matukio ya Afrika | DW | 10.04.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Silaha za Libya zatapakaa Mali, Syria

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linasema kuwa silaha zilizotumika kumng'oa madarakini rais wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi, mwaka 2011, sasa zinatumika katika mapigano katika nchi 12 zikiwemo Mali na Syria.

epa03444170 A Libyan government fighter checks his weapon as they advance towards the entrance to the town of Bani Walid, which is witnessing clashes between the army and some loyalists of the former Gaddafi regime, some 185 km south of the capital Libyan capital Tripoli, Libya, 23 October 2012. According to media reports on 22 October, the Libyan army has seized most of the south-eastern town of Bani Walid, where it is pursuing a campaign against rogue militias. The Libyan army on 20 October launched a massive-scale attack on Bani Walid after a siege of more than two weeks. EPA/STR +++(c) dpa - Bildfunk+++

Libyen Bani Walid Regierungstruppen

Timu ya waangalizi wa Baraza la Usalama iliyochunguza silaha za Libya imeripoti kuwa eneo la Afrika ya Kaskazini limekuwa ngome ya machafuko kwa kanda yote kwa tamaa ya waasi kuzing'oa serikali za nchi hizo, huku silaha za Libya zikitumika kwenye machafuko hayo.

Lakini Waziri Mkuu wa Libya, Ali Zeidan, aliliambia Baraza hilo la Usalama kuwa serikali yake haina uwezo wa kuzuia silaha hizo kutumwa Algeria, Niger, Tunisia, Chad, Sudan, Mali na Syria.

Silaha zinazotumika kama mabaki ya silaha zilizomtoa Gaddafi madarakani ni pamoja na silaha nzito na nyepesi, mabomu na maguruneti ambayo kwa sasa yanatumiwa kwa kiasi kikubwa nchini Mali na Syria.

Ripoti ya uchunguzi huo inaonesha kuwa Libya inachangia kwa kiasi kikubwa katika silaha hizo na kuwa juhudi zinahitajika ili kudhibiti silaha hizo kutotumika katika nchi nyingine za Afrika.

Miaka miwili ya kusambaza silaha

Mtoto wa Kilibya akibeba bunduki aina ya AK-47.

Mtoto wa Kilibya akibeba bunduki aina ya AK-47.

Ni miaka miwili sasa toka kuanza kwa usafirishaji wa silaha kutoka Libya kwenda nchini Syria ambako hutumika katika mapigano ya kupindua serikali ya Assad. Mapigano nchini Syria yamesababisha zaidi ya watu 70,000 kupoteza maisha. Usafirishaji silaha unatajwa kupangwa na watu wa ndani ya Libya kutoka miji ya Misrata na Benghazi, na kwamba silaha hizo hupitishiwa Uturuki na kaskazini ya Lebanon.

''Usafirishaji wa meli za silaha na vifaa vya kivitia kutoka Libya kwenda Syria unapewa baraka na serikali ya Libya, licha ya serikali hiyo kukanusha hilo,'' amesema afisa mmoja wa timu ya waangalizi wa silaha nchini Libya kwenye mazungumzo yake na shirika la habari la Reuters.

Amesema kuwa mwaka uliopita, Umoja wa Mataifa uligundua kiwango kikubwa cha silaha kilikuwa kikisafirishwa kutoka Libya kwenda Misri, hali inayotishia usalama na kanda nzima ya Afrika ya Kaskazini na Mashariki ya Kati.

Silaha hadi Misri

Raia wa Libya akikabidhisha bunduki yake kwa afisa wa jeshi katika kampeni ya kudhibiti silaha.

Raia wa Libya akikabidhisha bunduki yake kwa afisa wa jeshi katika kampeni ya kudhibiti silaha.

Mbali na silaha za Libya sasa kutumwa nchini Syria, kuna taarifa ya kuwa zinatumiwa katika vituo mbalimbali eneo la Sinai, Misri, na zingine kusafirishwa kwenda Ghaza kupitia mpaka huo wa Sinai.

Usalama katika mji wa jangwa wa Sinai ambalo linapakana na Israel, mji ambao ni kivutio cha utali Misri, ulichafuka hasa baada ya muamko wa wananchi wa Misri uliomtoa madarakani kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Hosni Mubarak, miaka miwili iliyopita.

Silaha zingine za Libya husafirishwa kupitia Kusini mwa Tunisia na Algeria pamoja na Kasikani mwa Niger kuelekea katika vituo mbalimbali nchini Mali huku silaha zingine zikibakia katika nchi ambazo zinapita ili kutumika katika mapigano ya ndani ya nchi hizo.

Waangalizi hao wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamedai kuwa baadhi ya silaha hizo zilikuwa zikitolewa na Qatar pamoja na Umoja wa Nchi za Kiarabu kwa ajili wa kuwasaidia waasi wa Libya kumuondoa madarakani Gaddafi katika mapigano ya mwaka 2011. Qatar na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu zikanusha kutoa silaha.

Mwandishi: Hashim Gulana/Reuters
Mhariri: Mohammed Khelef

DW inapendekeza