Waziri wa Ujerumani atoa mwito wa mshikamano
1 Desemba 2009Berlin.
Katika kuadhimisha siku ya ukimwi duniani leo, waziri wa afya wa Ujerumani Philipp Rösler ametoa mwito wa kujenga mshikamano na watu wenye maradhi hayo.Waziri Rösler amesema watu wanaougua maradhi ya ukimwi hawana haja ya kuona haya au kuficha maradhi yao.
Hatahivyo waziri huyo amesisitiza umuhimu wa kinga kwa kuwa bado tiba haijapatikana.
Katika kuadhimisha siku ya leo, madaktari na mashirika ya afya pia yametoa mwito wa kutenga fedha zaidi,kutoa elimu , na huduma za kuwalinda wanawake vizuri zaidi dhidi ya maambukizi.
Wakati huo huo Shirika la Afya Duniani,WHO limezitaka nchi zianze kuiondoa dawa ya ukimwi "Stavudine" hatua kwa hatua kwa sababu inasababisha madhara ya muda mrefu yasiyoweza kuondolewa.
Madhara hayo ni pamoja na kudhoofika na kupagaranyika kwa mishipa ya fahamu.