1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shirika la misaada ya kiutu OCHA kupunguza wafanyakazi 2,600

12 Aprili 2025

Shirika la Umoja wa Mataifa la misaada ya kiutu OCHA limesema linawapunguza wafanyakazi wake takriban 2,600 kwenye zaidi ya nchi 60 kutokana na uhaba wa fedha unaolikabili.

https://p.dw.com/p/4t3Vy
OCHA kupunguza wafanyakazi wake kutokana na uhaba wa fedha
Mkuu wa Shirika la Misaada ya Kiutu la Umoja wa Mataifa OCHA Tom Fletcher Picha: Denis Balibouse/REUTERS

Mkuu wa OCHA Tom Fletcher katika barua yake amesema bajeti ya OCHA inakaribia dola milioni 430 kwa mwaka lakini baadhi ya nchi zimepunguza michango yake kwa shirika hilo

Ameitolea mfano Marekani ambayo ni mfadhili mkubwa wa shirika hilo kuwa imeondoa mchango wake wa asilimia 20 sawa na dola za kimarekani milioni 63 iliyokuwa imetengewa mwaka huu wa 2025.

Soma zaidi: Mashirika yaunga mkono ombi la UN la dola bilioni 7

Fletcher, ameongeza kuwa kutokana na uhaba wa fedha unaolikabili shirika hilo, sasa linahitaji kubadilisha namna ya utendaji wa shuguli zake ili kuendana na rasilimali. Shirika hilo sasa litapunguza uwepo wake na kazi zake katika nchi za Cameroon, Colombia, Eritrea, Iraq, Libya, Nigeria, Pakistan, Zimbabwe na katika eneo la Gaziantep nchini Uturuki.