1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la droni lashambulia kinu cha nyuklia Ukraine

9 Aprili 2024

Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki limesema mlipuko uliotokea mapema leo ukidaiwa kusababishwa na shambulizi la droni katika kinu kikubwa kabisa cha nyuklia barani Ulaya ingawa hakuna kitisho cha moja kwa moja

https://p.dw.com/p/4eag0
Ukraine
Kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia nchini UkrainePicha: LIBKOS/AP/picture alliance

Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki limesema mlipuko uliotokea mapema leo ukidaiwa kusababishwa na shambulizi la droni katika kinu kikubwa kabisa cha nyuklia barani Ulaya sio kitisho cha moja kwa moja katika usalama wa kinu hicho. Hata hivyo, shambulizi hilo limeonyesha hatari kubwa inayokikabili kinu hicho. 

Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki limesema liliarifiwa kuwa mlipuko huo ulitokea mapema hii leo katika eneo la kituo cha mafunzo kilichopo karibu na kituo cha kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia.

Soma zaidi. Urusi: Ukraine imeshambulia kinu cha nyuklia Zaporizhzhia

Kituo cha Zaporizhzhia ni moja ya vinu 10 vikubwa vya nyuklia duniani. Mapigano yanayoendelea kusini mwa Ukraine yameibua hofu kwamba kuna uwezekano wa maafa ya nyuklia kama yale yaliyotokea Chernobyl mnamo 1986, ambapo kinu kililipuka na kusambaza miozi iliyoharibu eneo hilo.

Ukraine Krieg | Raketenangriff auf Saporischschja
Picha ya droni inayoonyesha athari ya shambulizi la Urusi katika mji wa Zaporizhzhia nchini UkrainePicha: Ivan Fedorov via Telegram/REUTERS

Katika miezi ya hivi karibuni sio Urusi wala Ukraine amabyo imeweza kusoga mbele zaidi katika uwanja wa mapambano kwa walau kilomita 100 katika upande wa kusini mashariki ingawa mashambulizi ya droni na makombora yameendelea kuvurumishwa katika vita hivyo.

Soma zaidi. Zelensky aliomba bunge la Marekani kuidhinisha msaada wa nchi yake

Mara kwa mara Urusi na Ukraine zimekuwa zikitupiana lawama za mashtaka juu kinu cha Zaporizhzhia. Siku ya Jumatatu, Moscow ilidai kuwa Ukraine ilikuwa nyuma mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye kituo hicho siku moja kabla, na Kyiv kuishutumu Urusi kuwa inatumia mbinu hizo ili kupotosha.

Watu 300,000 wangehama makazi yao

Kwa mujibu wa shirika la kutoa huduma za dharura nchini Ukraine ni kwamba shambulio hilo lingeweza kusababisha  maafa makubwa ambayo yangelazimu takriban watu 300,000 kuyahama makazi yao.

Ukraine
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa katika eneo liloshambuliwa na Urusi la ZaporizhzhiaPicha: Stringer/REUTERS

Soma zaidi.Ufaransa kujenga mahusiano yenye uwiano na Afrika

Wakati hayo yakiendelea, Rais wa Ukraine Vodymyr Zelensky amekagua ngome zake za kijeshi katika eneo la kaskazini mashariki la Kharkiv kutoa mwito wa kuomba msaada wa haraka wa kijeshi wakati Urusi ikizidisha mashambulizi yake ya anga katika eneo hilo.

UK
Waziri wa mambo wa nje wa Uingereza, David Cameron ameizuru Marekani kuishinikiza nchi hiyo kuisaidia UkrainePicha: JUSTIN TALLIS/AFP/Getty Images

Zelenskyy amekuwa akiyasisitiza mataifa ya magharibi kwamba waisaidiae nchi yake silaha zaidi ili iendeleze mapambano yake ya kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi, katika maelezo yake ameiasa pia Marekani kupitisha muswada wa dola bilioni 60 ambao umeshikiliwa na bunge la Marekani tangu mwaka uliopita na kwamba kama Marekani isipotoa msaada huo Ukraine itapoteza vita dhidi ya Urusi.

Kwa upande mwingine, waziri wa mambon ya nje wa Uingereza David Cameron yuko ziarani nchini Marekani kuishinikiza kambi ya chama cha Republican kuruhusu pesa hizo ambazo zinapaswa kupelekwa nchini Ukraine baada ya kukutana na rais wa zamani Donald Trump.

Cameron amesema ushindi kwa Ukraine ni muhimu kwa usalama wa Marekani na Ulaya lakini rais huyo wa zamani na anayetarajiwa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican ni mkosoaji wa msaada unaoendelea kutolewa na Marekani kwa Ukraine.