Serikali ya Kongo yapinga Chebeya kuzikwa Juni 30 mwaka huu
18 Juni 2010Matangazo
Mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu, Floribert Chebeya, ambaye alipatikana amekufa akiwa ndani ya gari lake mjini Kinshasa hapo tarehe 2 mwezi huu, atazikwa Jumamosi, tarehe 26 mwezi huu.
Mpango wa mazishi unafuatia hatua ya mwendesha mashataka mkuu wa taifa kuirejesha maiti ya Chebeya kwa familia yake baada ya kufanyiwa uchunguzi wiki iliopita na madaktari kutoka Uholanzi.
Hata hivyo, mashirika ya kutetea haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yameomba mazishi ya Floribert Chebeya yafanyike Juni 30, siku ambayo nchi hiyo itaadhimisha miaka 50 ya uhuru wake.
Taarifa kamili na mwandishi wetu wa Kinshasa, Saleh Mwanamilongo
Mwandishi, Saleh Mwanamilongo
Mpitiaji, Peter Moss
Mhariri, Othman Miraji