Serikali ya Italy ya Prodi yakabiliwa na changamoto baada ya waziri mmoja kujiuzulu | Habari za Ulimwengu | DW | 22.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Serikali ya Italy ya Prodi yakabiliwa na changamoto baada ya waziri mmoja kujiuzulu

ROMA:

Serikali ya Italy inayoongozwa na waziri mkuu Romano Prodi inayumbayumba kutokana na kujiondoa kwa mshirika muhimu wa serikali yake.-Waziri wa zamani wa sheria-Clemente Mastella amejiuzulu na kukiondoa chama chake kutoka kwa serikali wiki iliopita,baada ya kuchunguzwa kutokana na rushwa.Hatua hiyo imeiacha serikali ya ushirika ya Prodi bila ya wingi wa viti bungeni.Amefanya mkutano wa dharura na baraza lake la mawaziri na pia anatarajiwa leo kulihutubia bunge.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com