1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serengeti- Safari kuelekea kusikojulikana

17 Aprili 2014

Tunakupeleka pamoja nasi katika ulimwengu wa kuvutia: Jionee simba wanaounguruma, pundamilia wanaobweka na maelfu ya nyumbu - katika safari yetu ndani ya Serengeti.

https://p.dw.com/p/1BjzU

“Serengeti haitakufa“ – Filamu ya Bernhard Grzimek iliyoshinda tuzo ya Oscar haikuiweka tu Seregenti katika ramani, bali pia iliikuwa kama kioo cha maisha ya porini. Zaidi ya miaka 50 baadaye, mada zilizogusiwa katika filamu hiyo zina umuhimu kuliko ilivyowahi kutokea: Mabadiliko ya tabianchi, ujangili, magonjwa ya wanyama, na ongezeko kubwa la watu vinaitishia tunu hii. Serengeti iko hatarini.

Hata katika safari yake ya kwanza barani Afrika, Bernhard Grzimek alishtushwa na hali ya wanyamapori wa bara hili: “Dunia inazidi kuwa ndogo kwa ajili ya kulisha idadi kubwa na inayozidi kuongezeka ya watu. Hiyo ndiyo sababu idadi ya wanyama inapungua.” Mapema miaka ya 1950, mtafiti huyo wa wanyama alitambua tatizo kuu katika mbuga ya Serengeti: Kadiri idadi ya watu inavyozidi kuwa kubwa, ndivyo inavyozidi kuwa vigumu kuendeleza hali ya kuishi kwa kustahmiliana kati ya binaadamu na mazingira asili.

Wakati huo ni wachache sana katika taifa hilo lililokuwa koloni la Ujerumani katika Afrika ya Mashariki waliokuwa wanajihusisha na utunzaji wa mazingira ya asili. Tayari mbuga ya Taifa ya Serenegeti ilikuwepo, lakini mipaka yake ilikuwa karibu kubadilishwa. Grzimek aliiona hatua hiyo kama kitisho kwa wanyama katika mbuga hiyo. Lakini ni maeneo yapi yalikuwa muhimu hasa kwa wanyamapori? Grzimek na mtoto wake waliamua kuwahesabu wanyama kutokea angani – kwa ufanisi. Walimshawishi rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, juu ya umuhimu wa savana ya kaskazini mwa taifa hilo changa. Utunzaji wa Serengeti uliboreka, shukurani kwa kina Grzimek.