Rwanda na Ufaransa zafungua ukurasa mpya
25 Februari 2010Matangazo
Ziara hiyo inafanyika wakati ambapo Rwanda imeurejesha uhusiano wake wa kidiplomasia na Ufaransa baada ya kuuvunja miaka mitatu iliyopita.Rais Sarkozy anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame kwa mazungumzo na baada ya hapo watafanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.Kiongozi huyo wa Ufaransa alikuwa anatokea Mali alikokutana na rais Amadou Toumani Toure.Jee ziara hii ina umuhimu gani kwa Rwanda?
Mwandishi:Thelma Mwadzaya
Mhairiri:Mohamed Abdul-Rahman