1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Rais Xi Jinping wa China aanza ziara barani Ulaya

5 Mei 2024

Rais wa China Xi Jinping amewasili siku ya Jumapili mjini Paris nchini Ufaransa, kuanza ziara yake rasmi na ya nadra barani Ulaya katika safari ambayo itampeleka pia Hungary na Serbia.

https://p.dw.com/p/4fWCN
Rais wa China Xi Jinping
Rais wa China Xi JinpingPicha: Yomiuri Shimbun/AP/picture alliance

Siku ya Jumatatu, Xi atakutana kwa mazungumzo na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pamoja na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen.

Kulingana na taarifa ya Ikulu ya Elysée, mazungumzo kati ya Rais Macron na Xi, yatajikita zaidi katika masuala ya ushirikiano wa kiuchumi, mizozo inayoendelea duniani ikiwa ni pamoja na vita vya Ukraine na Mashariki ya Kati. Awali, Macron alisema ni lazima China ihusishwe katika masuala makubwa ya kimataifa.