Rais Obama na mkakati mpya kuhusu hali nchini Afghanistan | Matukio ya Kisiasa | DW | 30.09.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Rais Obama na mkakati mpya kuhusu hali nchini Afghanistan

Rais Barack Obama wa Marekani leo atakutana na washauri wake wakuu, kubadilishana mawazo iwapo mkakati mpya nchini Afghanistan unahitaji mabadiliko.

default

Rais Barack Obama wa Marekani

Kamanda mkuu wa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan, Generali Stanley McChrystal aliwasha moto pale ripoti yake ya siri ilipofichuka akionya kuna uwezekano mkubwa wa Marekani kushindwa nchini Afghanistan, katika mwaka mmoja ujao, iwapo hawataongeza idadi ya wanajeshi.

Ishara ya umuhimu wa mkutano, huo na usiri wake inajitokeza wazi, ukiangalia orodha ya waliopata mualiko na eneo mkutano huo unafanyika. Eneo ni chumba chenye usalama mkuu katika Ikulu ya Marekani.

Mkutano huo unaolenga kutathmini mkakati wa Marekani nchini Afghanistan, na wapi panapohitajika mabadiliko, hasa kuhusiana na swala la kuongezwa kwa idadi ya wanajeshi, maamuzi yake yatachangia iwapo Marekani itakuwepo Afghanistan kwa muda mrefu.

Rais Obama atakaa mezani na washauri wake wakuu, ikiwemo, Makamu wa rais Joe Biden, Waziri wa mambo ya nchi za nje Hillary

Hillary Clinton

Waziri wa mambo ya nchi za nje Bibi. Hillary Clinton

Clinton, na Robert Gates anayesimamia wizara ya ulinzi.  Generali Stanley McChrystal, kamanda mkuu wa majeshi ya Marekani Afghanistan, pia anasemekana atahudhuria au kama sivyo atashiriki katika majadiliano hayo kwa njia ye video.

Rais Obama amekuwa na shinikizo nyingi, kubadili mweleko nchini Afghanistan, na hasa baada ya ripoti ya McChrystal kufichuka. McChrystal alikuwa anaonya katika muda wa mwaka mmoja ujao, Marekani huenda ikashindwa huko Afghanistan iwapo haitaongeza idadi ya wanajeshi. McChrystal anasemekana ameitisha wanajeshi wengine kiasi cha elfu 40 kukabiliana na uasi wa Taliban unaozidi.

Mkakati Afghanistan pia ulikuwa ndio ajenda katika mkutano wa Rais Obama na katibu mkuu wa Nato, Anders

NATO-Generalsekretär Anders Fogh Rasmussen

Katibu Mkuu wa NATO Jenerali Anders Fogh Rasmussen

Rasmussen katika ikulu ya Marekani- alipoashiria kuwa Marekani inahitaji ushirikiano zaidi kutoka nchi za Ulaya.

Washirika wakuu wa Marekani Ulaya bado wana shaka, hasa kuhusiana na kuongeza idadi ya wanajeshi, Afghanistan. Jana Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani, Franz Josef Jung, alisema  washirika wa

Deutschland Bundesverteidigungsminister Franz Josef Jung

Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung

NATO barani Ulaya wanafaa, kusubiri hadi pale Marekani itakapotoa mpango rasmi wa kuongezwa kwa wanajeshi Afghanistan.

Anders Rasmussen lakini alimhakikishia rais Obama kuwa majeshi ya NATO Afghanistan yataendelea kuwepo , hadi watakapokamilisha kazi iliyowapeleka nchini humo.

Kura ya maoni nchini Marekani zinaashiria kuwa Wamarekani wengi wamepoteza imani na vita hivyo Afghanistan. Ni changamoto hizi ndizo Rais Obama ataendelea kupima kabla ya kufanya maamuzi, wa mkakati ufaao nchini Afghanistan.

Mwandishi: Munira Muhammad/AFPE

Mhariri: Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com