UchumiUfaransa
Macron aitahadharisha Ulaya kuhusu makabiliano na Marekani
10 Februari 2026
Matangazo
Katika mahojiano yaliyochapishwa kwenye magazeti kadhaa ya Ulaya, Macron amesema Ulaya haipaswi kujidanganya na utulivu katikati ya mvutano na Washington kama mabadiliko ya kudumu licha ya kile kinachoonekana kama kumalizika kwa misuguano kuhusu Greenland biashara na teknolojia.
Amesema, utawala wa Trump umekuwa "ukiipinga waziwazi Ulaya" na unataka Umoja wa Ulaya kusambaratika.
Viongozi wa Ulaya watakutana mjini Brussels siku ya Alhamisi kwenye mkutano wa kilele ambapo watajadili hatua za kuimarisha uchumi wa umoja huo na kuifanya iweze kusimama kidete dhidi ya Marekani na China katika ngazi ya kimataifa.